DALILI ZA HIV ZA MWANZO NA DALILI ZA UKIMWI ZA MWANZO

Kama ilivyo magonjwa mengi hupitia hatua kadha kadha na kuonyesha dalili kadha katika hatua hizo. Basi HIV nayo ina hatua zake mpaka kuwa UKIMWI.

DALILI ZA MWANZO ZA HIV AMA UKIMW
Dalili hizi huanza kuonekana kuanzia wiki mbili mpaka nne na wakati mwingine mpaka sita toka kuingia mwilini. Mara chache sana huweza kuonekana mwanzoni mwa wiki ya kwanza. Katika kipindi hiki mtu anaweza kuona dalili zifuatazo:
1.kufimba kwa tezi za kwenye makwapa, mapaja na shingo
2.Homa
3.Uchovu
4.Kuharisha
5.Kupungua uzito
6.Kikohozi
7.Pumzi kutoka kidogodogo
8.Mafua


Dalili hizi pia zinaweza kuhusiana na maradhi mengine, hivyo inaweza kuwa vigumu kujuwa nini chanzo zaidi. Wengi katika wanaopata HIV wametaja kuwa kuvimba kwa tezi ndio dalili pekee walioweza kuopata mwanzoni mwa kuathirika kwao. Wengine wanataja mafua kuwa ndio dalili yao ya kwanza.

Baada ya kipindi hiki kupita mgonjwa hatapata dalili yeyote ile. Hiki ni kipindi hatari sana kwani mtu hataweza kujijua kama ameathirika. Kipindi hiki kinaweza kudumi mpaka miaka 10. katika kipindi hiki virusi vinaendelea kuathiri seli za mwili. Baada ya mwili kuwa umeathirika sana na kudhoofu mtu ataanza kupata dalili za UKIMWI.

DALILI ZA UKIMWI
1.kutokwa na jasho jingi wakati wa usiku
2.Kupata homa za mara kwa mara na kuhisi baridi
3.Kikohozi
4.Kushinwa kupumua vyema
5.Madoa madoa kwenye ulimi na mdomoni
6.Maumivu ya kichwa
7.Uchovu usiokuwa na sababu na usioisha
8.Kutokuona vyema
9.Kupungua uzito
10.Mapele na ukurutu kwenye ngozi