YEAR OF JUBILEE (MWAKA WA MAACHILIO au MWAKA WA UBWETE-UBWETE)
IBADA YA MKESHA WA MWAKA MPYA 2022 KATIKA KANISA LA EFATHA MWENGE DAR ES SALAAM TANZANIA.
MCHUNGAJI BETSON KIKOTI.
NENO LA SHUKRANI.
Isaya 12”1-6 “Na katika siku hiyo utasema, Ee Bwana, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo……...”
Mungu alikuwa amepata hasira kwa ajili ya watu wake lakini baada ya Mungu kugeuza hasira yake ndipo Isaya akamshukuru Mungu, hasira ya Mungu iligeuzwa kwa sababu Mungu anawapenda watu wake, katika miaka saba ambayo tumetembea nayo sisi wana Efatha hasira ya Mungu iligeuzwa kwa sababu Mungu anatupenda. Katika yale tuliyopitia ili tufikie mahali pa ushindi Mungu amegeuza hasira yake kwetu ili sisi tupate kusonga mbele, tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya hilo, mwaka 2022 utakuwa ni mwaka wa matumaini na wa kheri kwetu, kwa sababu hiyo tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu.
Mtu ambaye amemwamini Mungu na anafuata utaratibu na majira yake kamwe hatapotea bali atakuwa salama katika Yeye.
Mungu aliwaambia wana wa Israel kuwa kila mwaka wa saba kutakuwa ni mwaka wa maachilio, kusameheana na ni mwaka wa Baraka, hivi ndivyo ilivyo kwetu sisi wana Efatha, mwaka wa 2022 ni mwaka wetu wa saba wa Mtembeo wa Mungu hivyo utakuwa ni mwaka wa kubarikiwa, ni mwaka wa kusameheana na ni mwaka wa kupokea Baraka.
HAPPY BIRTHDAY DADDY - PRESIDING APOSTLE & PROPHET JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA.
0 Comments
Post a Comment